skip to main |
skip to sidebar
FAIZA ALLY: NATAMANI KUHONGWA KWA SABABU SIJAWAHI
Muigizaji na mrembo mwenye vituko kibao, Faiza Ally, amesema atafurahi
sana endapo atampata mtu wa kumuhonga kwa sababu hajawahi kuhongwa hata
siku moja. Akizungumza kupitia kipindi cha Kubamba cha Times Fm, Bi dada huyo
mwenye mtoto mmoja amedai ameanzia mbali kutafuta fedha na karibu... kila
kitu chake anajihudumia mwenyewe.
“Natamani nipate mtu wa kunihonga, coz mimi kila kitu najifanyia
mwenyewe, hata biashara yangu nmeisimamisha mwenyewe nilishawahi hata
kuuza mama ntilie” Alisema. Katika hatua nyingine muigizaji huyo ambaye anategemea kuiingiza sokoni
filamu yake mpya muda si mrefu, ameweka wazi kuwa amenunua gari ya ndoto
yake aina ya Landrover.
0 comments:
Post a Comment