Kupitia ukurasa wake wa instagram staa huyo wa single ya “Back to sleep”ali-post picha inayoonyesha mchoro wa sura ya mwanae Royality na kuandika…. ‘I do what the f*** I want.’
.
Royality ni binti na mtoto pekee wa Chris Brown aliezaa na mwanamke anaefahamika kama Nia Guzman,kitendo kilichopelekea Mwanamuziki huyo kutengana na aliekua mpenzi wake ambae pia ni mwanamitindo Karruche Tran mapema mwaka jana,baada ya mwanamitindo huyo kubaini kuwa Chris Brown ni baba wa mtoto huyo.
Hata hivyo mapenzi ya Mwanamuziki huyu kwa mtoto wake hayajaanzia kwenye mchoro huu wa ‘tattoo’ kwani mwezi August 2015,Breezy alitangaza kuachia album yake mpya aliyoipa jina la mwanae “Royality”ambapo kwenye artwork-cover ya album hiyo,ilimuonesha Chris Brown akiwa amembeba mwanae.
Hata hivyo miezi ya hivi karibuni kumekua na mgogoro kati ya Chris Brown na Mama wa mtoto huyo,mara baada ya mwanamke huyo kumfikisha mahakamani akipinga mwanamuziki huyo kumlea binti yao kwa madai kuwa Brown amekua akijihusisha na vurugu na matumizi ya madawa ya kulevya kama ‘bangi’,ambapo mahakama ilitupilia mbali madai hayo na kumpa Chris Brown uhuru wa kukaa na binti yake kwa siku 12 kila mwezi,na kutakiwa kumlipa Mama wa mtoto huyo kiasi cha dola $2,500 kila mwezi kama malipo ya malezi (child support allowance),huku jina la binti huyo likibaki kuwa Royality Brown.
0 comments:
Post a Comment