Pages

Subscribe:

Thursday, October 6, 2016

CHIRSTIAN BELLA: MIMI SIYO MSANII WA BONGO FLAVA, DANCE, TAARAB WALA R&B

bella
Mwanamuziki Christian Bella amedai utakuwa unamkosea ukimwita yeye ni msanii wa muziki wa bendi au msanii wa muziki wa bongofleva kwa kuwa anafanya muziki wa aina nyingi. Mkali huyo wa masauti ambaye anafanya vizuri na wimbo ‘Nishike’, Ameda kuwa yeye ni mwanamuziki kwa kuwa anafanya vitu vingi ndani ya muziki.

“Mimi ni msanii ninayefanya muziki ndani ya Tanzania, sio muziki wa bongofleva, sio muziki wa dansi, sio msanii wa taarabu,” alisema Bella “Mimi ni mwanamuziki, mimi ni mwanamuziki kwa...
ujumla, usiniseme mimi ni Bella msanii wa muziki wa dansi au Bella msanii wa muziki wa bongofleva au Bella msanii wa taarab au Bella msanii wa R&B, Christian Bella ni mwanamuziki,”

Aliongeza “Mimi nafanya muziki kufurahisha kila mtu, nafanya muziki kufurahisha wanahip hop, wana bongofleva, wana dansi,wana taarab ndio maana mimi naitwa mwanamuziki,”
Pia muimbaji huyo amewataka mashabiki wa muziki wake kukaa makao wa kula kwa ajili ya ujio wa studio yake pamoja na label ya kusimamia wasanii.

0 comments:

Post a Comment