Msanii wa bongo fleva, Nuh Mziwanda amefunguka kwa kudai chanzo cha
kuvunjika kwa ndoa yake ni kutokuwa na pesa za kutosha za kuweza
kuwahudumia familia ya mke wake kama alizokuwa nazo mwanaume aliyemuoa
Nawal hivi karibuni.
Nuh
Mziwanda amebainisha hayo, baada ya kila kitu mtu kutamani kujua chanzo
cha kuvunjika ndoa yao ni kipi, kutokana wawili hao wamekaa kwa...
muda wa
mchache kwenye ndoa hiyo kwa takribani miezi mitano huku akijitetea
kuwa hajawahi kumuacha mke wake japo walikuwa na migogoro mingi ndani ya
nyuma yao.
"Sijaachana na mke wangu
Nawal kwa sababu bado sijatoa talaka mpaka muda huu kusema simtaki
aendelee na maisha yake, japo kulikuwepo na msuguano wa hapa na pale
ambao naamini haukuwa unatokana baina yetu, bali ulikuwa unataka na
famili yake", alisema Nuh Mziwanda.
Pamoja na hayo, Nuh aliendelea kwa kusema "Nawal
hajawahi kuniambia mimi na yeye basi tuachane, ila
ninavyokumbuka alinipigia simu siku chache kabla ya kuolewa akitaka
talaka yake wakati yupo nyumbani kwa wazazi wake.
Maana alikuwa anapenda
sana maamuzi ya kukimbilia kwao kila tunapopishana kwa hata jambo ndogo
pamoja na kutaka talaka sasa sijui kwa sababu jamaa aliyemuoa ana uwezo
wa kifedha kwamba anaweza akazungusha 'mkwanja' pale 'home' kwao", alisema Nuh Mziwanda.
Kwa upande mwingine, Nuh Mziwanda
alisema aliamua kubadili dini yake na kuingia katika uislamu ni kutokana
na kuwa alimpenda sana Nawal kwa kuwa ni mwanamke pekee aliyeweza
kubeba ujauzito kati ya wanawake wote aliyokuwa nao kabla ya kufunga
naye ndoa kwa mara ya kwanza.



Follow on Instagram
0 comments:
Post a Comment