Msanii Zuwena Mohamed 'Shilole' amekanusha zile tetesi zilizokuwa
zinamuandama za kuiba mume wa mtu na kudai jambo hilo halina ukweli ila
watu wamezoea kumuongelea vibaya kwa kuwa yeye ni mtu maarufu.
Shilole
amefunguka hayo baada ya kuandamwa takribani majuma mawili hivi sasa
kuwa amevunja ndoa ya mwanamke mwenzake na hatimaye...
kumchukua mwanaume
huyo jumla jumla na kukaa naye nyumbani kwake jambo ambalo lilipelekea
watu wengi kumtolea maneno kwenye mitandao ya kijamii.
"Siyo kweli, sijawahi kuiba
mume wa mtu mimi. Ila huyo mwanaume ni kweli alikuwa na mke lakini
walisha achana siku nyingi hivyo kuwa naye siyo sababu ya kuivunja ndoa
yao", alisema Shilole.
Pamoja na hayo, Shilole ameendelea kwa
kusema kuwa anatarajia kuolewa siku si nyingi kutokea sasa japo
hakutegemea jambo hilo kutokea kwake tena.
"Panapo majaliwa nategemea
kuolewa mwezi wa 10 au 11 mwaka huu haupinduki lazima ntakuwa nimeolewa.
Kiukweli sikutamani kabisa kuolewa kwa sababu nilishaufunga ule ukurasa
lakini imetokana tu ushawishi wa mwanaume niliyekutana naye. Wakwe
zangu wamenipokea vizuri siku nilivyotambulishwa na wamenipenda kiukweli
kwa kuwa mimi nipo vizuri kila sehemu", alisema Shilole.
Katika hatua nyingine, Shilole amewataka
watu watambue kuwa yeye siyo chanzo cha migogoro ya kuvunjika kwa ndoa
ya mpenzi wake wa zamani Nuh Mziwanda kama watu wanavyodhani.
"Mimi kiukweli siyo chachu
ya ndoa ya Nuh Mziwanda na Nawal kuvunjika hata kidogo kila mmoja ana
mambo yake anafanya lakini nashangaa kwanini nahusishwa mimi kwenye
mambo yao yakitokea, maana hata wakigombana chumbani wanasema mimi ndiyo
chanzo. Siyo sawa kiukweli maana yameshapita ile kitu lakini nashangaa
bado kuendelea kuwepo kwenye midomo ya watu", alisisitiza Shilole.
Kwa upande mwingine, Shishi amedai hata
akiolewa hatoweza kubadilika kwa kuwa kazi yake haiwezi kuingiliana na
ndoa yake hata siku moja



Follow on Instagram
0 comments:
Post a Comment