Pages

Subscribe:

Tuesday, October 10, 2017

HATMA YA MESSI NA KIKOSI CHAKE KUJULIKANA KESHO


Alfajiri ya Jumatano michuano ya kufuzu kwa fainali za kombe la dunia mwaka 2018 kwa bara la America Kusini itaendelea na michezo mitano inapigwa katika viwanja tofauti na hizi zikiwa mechi za mwisho.

Timu 6 zina tiketi kwenda Urusi huku moja tayari wana tiketi na timu 3 hazina matumaini, lakini mchezo ambao unavuta hisia za wapenda soka wengi itakuwa kati ya Argentina na...
Ecuador.

Mchezo huu umetajwa kuwa na msisimko wa aina yake kwani unaweza ukaamua kuhusu hatma ya Argentina iliyo sheheni nyota wengi akiwenk Lioneil Messi, mchezo huu unaweza ukaipeleka Argentina kombe la dunia au wakakwama kama ilivyokuwa 1970.

Argentina watacheza mchezo huo huku wakiomba mchezo kati ya Peru na Colombia ambao wanashika  nafasi za juu wafungane au pia wakitoka suluhu itawasaidia kufuzu.
Ushindi tu ndio matokeo yanayohitajika leo kwani Paraguay nao wanaweza kufuzu endapo Peru na Colombia watasuluhu huku wao wakiwapiga vibonde Venezuela.

Lakini hata Uruguay walioko nafasi ya pili hawana uhakika kufudhu kwani kama watafungwa na Bolivia hii leo, Colombia, Chile na Argentina wakashinda itawapeleka kutoka bafasi ya pili hadi tano.

Chile walioko nafasi ya tatu, wenyewe nao wanahitaji ushindi ili kufudhu kwa michuano hiyo mikubwa dunia, hii leo Chile wataikabili Brazil lakini pia kama Peru na Colombia watatoka sare baasi itawashuhudia Chile wakipeta.

Colombia wanatakiwa kuifunga Peru kama wanahitaji kwenda Urusi lakini vilevile kama Chile wakipigwa na Brazil huku Argentina wakifungwa na Ecuador baasi Colombia watakuwa na nafasi.

Kiujumla ni mataifa matatu tu ambayo hayana nafasi kufudhu kwa fainali za kombe la dunia toka ukanda huu, mataifa hayo ni Ecuador,Bolivia na Venezuela huku kinara Brazil tayari wana uhakika kwenda kombe la dunia

0 comments:

Post a Comment