Watu wasiofahamika wameshambulia watu kwa risasi kwenye tamasha la
muziki katika jimbo la Las Vegas nchini Marekani, na watu 50 kuuawa huku
zaidi ya 200 wakijeruhiwa.
Tukio hilo limetokea usiku wa jumapili, ambapo milio ya risasi ilianza kusikika eneo la 'Mandalay Bay Resort and Casino' Las Vegas wakati tamasha la muziki likiendelea, huku msanii...
wamuziki wa Country Jason Aldean akiwa anaburudisha.
Polisi wa Las Vegas nchini Marekani wamesema wamefanikiwa kumuua mshukiwa mmoja ambaye inasemekana ni mkazi wa eneo hilo, huku wakimtafuta mwanamke mmoja ambaye alikuwa anaongozana naye, aliyejulikana kwa jina la Marilou Damley
Imeelezwa kwamba mtu huyo aliyeuawa ndiye aliyekuwa akifanya shambulizi hilo, na hivyo hakuna hali ya hatari tena kwa wakazi wa eneo hilo.
Askari polisi wawili ambao hawakuwa zamu ni miongoni mwa watu waliojeruhiwa, na tayari wamekimbizwa hospitali kwa ajili ya matibabu.

0 comments:
Post a Comment