Tuesday, August 8, 2017
AUGUST 13 FID Q KUJA NA KITU HIKI KIPYA
Msanii wa hip hop Bongo, Fid Q amesema huenda August 13 akatoa albamu yake ya tatu.
“Kuna uwezekano tukatoa albamu August 13 katika hatua za mwisho za kukamilisha mambo, pia tunaweza tukaachia na ngoma tatu tuendelee...
kuombeana dua na tuwe pamoja,” Fid Q amesema hayo alipokuwa akizungumza na Bongo5.
Fid Q ameongeza kuwa, “albamu inafahamika jina lake na mashabiki wanajua, albamu yangu ya kwanza inaitwa Vina Mwanzo Kati Na Mwisho, albamu ya pili inaitwa Propaganda, ya tatu ambayo inasubiriwa kutoka inaitwa Kitaa Olojia,” amesema.
August 13 imekuwa ni siku muhimu kwa rapper huyo kwani ni siku ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwake, hivyo amekuwa akiifanya ya kipekee zaidi.
Labels:
HABARI & UDAKU
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment