Darassa ametangaza kuachia kazi yake mpya ndani ya mwezi huu wa nane ambayo kwa mujibu wa kile alichoanza kuweka kwenye mitandao ya jamii huenda kazi hiyo ikaitwa...
'Hakuna Wasiwasi".
Darassa mwishoni mwa mwaka jana aliachia wimbo wake 'Muziki' ni wimbo ambao ulileta mapinduzi makubwa katika muziki wa Bongo fleva hususani kwa wasanii wa Hip hop kwani uliweza kuwa wimbo maarufu zaidi kwa muda mrefu, huku ukichezwa kila kona na kuimbwa na kila rika ndani ya nchi hata nje ya nchi.
Muziki ni video ya kwanza kwa wasanii wa Hip hop Bongo ambayo mpaka sasa imetazamwa na watu wengi kwenye mtandao wa You Tube kwani imefikisha watazamaji zaidi ya milioni tisa.



Follow on Instagram
0 comments:
Post a Comment