Pages

Subscribe:

Tuesday, August 22, 2017

FID Q: WANA VIEWS WENGI YOUTUBE ILA TUKIKUTANA KWENYE SHOW HUWA NAWAKALISHA


Msanii wa muziki wa hip hop Bongo, Fid Q amedai idadi ya views katika mtandao wa YouTube si kipimo katika muziki wa hip hop Bongo.

Rapper huyo ambaye kwa sasa anafanya vizuri na ngoma zake mbili mpya ‘Fresh na Ulimi Mbili’, ameiambia FNL kuwa idadi ya viewers mara myimgi huenda kinyume na...
uhalisia.

“Kwanza nafikiri nyingi hazipati (views) hizo kwa sababu wana hip hop ni watu ambao huwa tunatoa ngoma na zinakuwa zimefika. Unajua views na mambo ya YouTube sometimes hayamati sana katika uhalisia, huwa tunakutana na watu ambao wana-views milioni na kadhalika katika show na tunakuwa kama sisi ndio tuna hizi views milioni,” amesema na kuongeza.

“Kwa hiyo huwa nawaambia watu kila siku kwamba number do lie sometime, kwa sababu unaambia mbili jumlisha mbili ni nne na mbili mara mbili ni nne lakini mbili toa mbili ni sifuri,” amesisitiza.
Ngoma mpya Fid Q ‘Fresh’ ambayo aliitoa August 13 mwaka huu hadi sasa ina views 160,646 katika mtandao wa Youtube.

0 comments:

Post a Comment