skip to main |
skip to sidebar
GIGY MONEY: BARNABA NI KAKA YANGU PIA SHEMEJI YANGU
Baada ya Gigy Money na Barnaba kupiga picha wakiwa wamepakatana na
kuzua gumzo kwenye mitandao ya kijamii wakidaiwa kwamba ni wapenzi,
Elias Barnaba ‘Barnaba’ na muuza sura Gift Stanford ‘Gigy Money’
wameibuka na kudai kuwa wao si wapenzi.
Awali kulikuwa na nyepesinyepesi
zikidai kuwa hiyo haikuwa mara ya kwanza kwa wawili hao kuonekana
wakiwa wamepakatana katika...
maeneo mbalimbali, wakisema baada ya Barnaba
kuachana na mkewe, aliamua kujiweka kwa mwanadada huyo asiyeishiwa
matukio mjini.
Za Motomoto
News ilipowasiliana na Barnaba, alisema Gigy Money ni dada yake kama
walivyo madada wengine na katika maisha yake haishi kwa skendo hivyo
wanaosema hivyo siyo kweli.
Kwa upande wake Gigy, alisema Barnaba ni kaka yake na pia shemeji
yake, kwani ni rafiki wa aliyekuwa mpenzi wake, Mo J na hiyo picha
walipigwa wakiwa kwenye shoo hivyo hakuna suala la mapenzi kati yao.
0 comments:
Post a Comment