Pages

Subscribe:

Friday, August 11, 2017

JUMA NATURE: GIGI MONEY BADO MDOGO SANA AFANYE MAZOEZI

Msanii Juma Nature amewakingia kifua wasanii wa kike wa zamani ambao Gigy Money amesema walikuwa hakuna cha maana wanachokiimba, na kumtaka atulie kwani bado ni mdogo kwenye tasnia. 

Akizungumza na mwandishi Juma Nature amesema kitu ambacho Gigy Money anatakiwa kufanya sasa hivi ni mazoezi ili aweze...
kuandika nyimbo, na sio kuongea hovyo kuponda watu wazima, kwani hajapitia mikiki kwenye maisha ya muziki.

"Hawezi kuwa na dharau wakati mtu mwenyewe hata albam saba hajafikisha, bado mdogo sana afanye mazoezi atunge nyimbo zenye hekima, anaweza akapata matuzo kibao, lakini asiongee ongee hovyo bado mdogo sana huyo mtoto, hajawahi kupata mikiki, aingie kwenye mikiki mikiki awaulize wenzake kina Zay B  watamfundisha wanawake wenzake, sisi wanaume kwetu ndiyo asiingie kabisa kwa sababu huku vitani", alisema Juma Nature.

0 comments:

Post a Comment