Pages

Subscribe:

Friday, August 4, 2017

MENEJA MANENO: NAWEZA KUMTENGENEZA STAR NA AKAWA STAR ZAIDI


Msanii wa muziki wa kizazi kipya Meneja Maneno amewashangaa watu wanaomponda kuwa anatafuta umaarufu, na kusema yeye tayari ni maarufu kwani yeye ni star wa mastar. 

Akizungumza kwenye Planet Bongo ya East Africa Radio, Meneja Maneno amesema huwezi kumuita yeye ni msanii chipukizi kwani yupo kwenye game kitambo na ameshawatoa...
wengi kupitia yeye.

"Huwezi kuniita mimi underground, mi ni star wa mastar, kama nimeweza kumtengeneza star na akawa star, na kama nikatoa kitu kikaweza kufanza zaidi ya bongo star search, mi ni zaidi ya hao mastar", alisema Meneja Maneno. 

Meneja Maneno amewahi kuwasimamia baadhi ya wasanii wa muziki hapa nchini na kufanikiwa kutoka, lakini kwa sasa na yeye ameamua kuingia studio na kutoa ngoma ambazo zimefanya vizuri hewani.

0 comments:

Post a Comment