Pages

Subscribe:

Friday, August 4, 2017

MSAMI APIGA MAGOTI KWA UWOYA NA KUDAI NI MTU MUHIMU KWAKE

Baada ya Msami kutibua mambo ndani ya FNL kwa kusema kuwa yeye alitongozwa na muigizaji Irene Uwoya, msanii huyo amejishusha na kumtaka radhi muigizaji huyo kwa kauli hiyo ambayo aliitoa hadharani. 

Akifunguka kwenye mahojiano na  eNewz ya EATV, Msami amesema kuwa haitaji kuwa na uadui na muigizaji huyo kwani licha ya kuwa kwenye mahusiano kwa muda mrefu na kutengana, lakini bado wanasaidiana na...
Uwoya ni mtu muhimu kwenye maisha yake.

"Irene ni mshikaji wangu sana. Hata baada ya kuachana bado tunasaidiana sana. Mimi sipendi unapotengana na mtu halafu ukaanza kuonyesha kwa watu kuwa tumeachana haijengi picha nzuri kwani huzaa chuki. Kwa kauli yangu niliyoitoa kama nilimkwaza mtu nakiri kwamba naomba msamaha. Nilikosea sana na sikudhamiria kumuumiza mtu. Irene ni mtu poa sana na haiwezi kutokea hata siku moja mimi nikaja kusema kwamba uwoya alikuwa mbaya kwangu," Msami.

Pamoja na hayo Msami ameongeza kuwa "Nataka kutengeneza fan base yangu napenda mashabiki wa Uwoya waendelee kunisapoti muziki wangu na mimi mashabiki zangu waendelee kushabikia kazi za uwoya na siyo chuki.

Baada ya Msami kukiri mbele ya kipindi cha FNL Ijumaa ya tarehe 28 Julai kulikuwa na maneno yaliyoendelea kupitia mtandaoni huku ikisadikika ni madongo kwenda kwa Msami kutokana na kujisifu hakuwai kumtaka kimapenzi Irene bali yeye alitongozwa.

"Dogo Janja kutoka kimapenzi na Irene haijanishangaza au kunifanya mimi nipotee kwenye game kwa sababu kwenye mapenzi mimi sijawahi kuachika bali huwa naachaga. Uwoya yeye ndiye alinitongoza mimi kwani sijawahi kumtongoza ........" Hii ni kauli ya Msami akiwa FNL.

0 comments:

Post a Comment