Msanii wa Hip hop Hamis Mwinjuma a.k.a Mwana FA ameshindwa kutimiza ahadi ambayo aliitoa kwa mashabiki wake miezi 7 iliyopita kwamba video yake 'Dume suruali' itakapofikisha jumla ya watazamaji milioni tatu basi angeachia ngoma nyingine.
kuwa na mafanikio ya juu kwenye mitandao ya kijamii hususani You Tube.
Novemba 25, 2016 Mwana FA aliachia video ya 'Dume Suruali' na ilipofika Januari 11, 2017 ilikuwa imefikisha jumlaa ya watazamaji milioni moja kitu ambacho kwa Mwana FA kilikuwa ni kikubwa na yeye alikiri kuwa si jambo la kawaida kwake.
"Najua kwa baadhi ya wasanii
hii siyo namba kubwa hata,ila kwangu 'its a big deal' sababu haijawahi
kufika kamwe! nawashukuru sana, salutes nyingi, heshima kwenu,
ninyoosheni kwa kuifikisha angalau milioni mbili ama tatu nizidi
kuwakubali tafadhali endeleeni kuangalia mnikomoe" aliandika Mwana FA kupitia Instgram yake
Tarehe 16 Januari video hiyo ilifikisha watazamaji milioni mbili jambo ambalo lilimfanya Mwana FA kuwa na furaha zaidi na hapo ndipo alipotoa ahadi akiwa na furaha na kusema labda ngoma hiyo ikifikisha watazamaji milioni tatu angeweza kuachia ngoma nyingine.
"Najua kwamba siyo namba
kubwa hii kwa baadhi ya wasanii, 'actually' ni kanamba flani kaduchu
tu,ila kwangu 'its a big deal' kwa hivyo sitakaa niigize hapa kuwa 'this
is how we do it' na 'it's normal', no it's not, siyo
kawaida..Nashangaa, ahsanteni sana. 'how about tukifika 3 milioni
tunatoa ngoma nyingine? now lets get to 3 milioni" alisisitiza Mwana FA kupitia ukurasa wake wa Instgram



Follow on Instagram
0 comments:
Post a Comment