Rapa Mwana FA, a.k.a The Choir Master amewataka wasanii wenzake wawe na
mapenzi ya dhati katika kile wanachokifanya ili kiweze kuwaletea
manufaa zaidi nasiyo kutegemea kiki kuliko muziki wao.
Mwana
Fa amebainisha hayo baada ya wasanii wengi kufahamika zaidi kupitia
skendo mbalimbali kuliko hata...
muziki wake ambao anaoufanya kama kazi
yake kila siku.
"Kitu cha kwanza
ninachokitaka kwa wanamuziki wawe na mapenzi na muziki, maana tunakosea
sana tunavyofanya muziki biashara kwa kutegemea muziki utuletee pesa tu
na umaarufu bila ya kuwa na mapenzi kwenye muziki wenyewe. Ndiyo maana
tunaona makiki yanazidi kuliko muziki tunaofanya, yaani watu wanafanya
matukio yanawapa umaarufu lakini ukija kuulizia kazi zake huzijui
alizofanya", alisema Mwana FA.
Pamoja na hayo, Mwana FA amesema kwa
upande wake aina ya muziki anaoufanya ndiyo unapelekea kutofanya
'collabo' nyingi na wasanii wa kimataifa.
"Naamini kuna soko kubwa
sana hapa Tanzania, naona jinsi nguvu nyingi zinazotumika kujaribu labda
kuupeleka muziki wetu nje ya mipaka yetu. Siwezi kurizika hili ni soko
langu naamini hata bado sijalimaliza, soko letu lipo hapa hapa hizi
nyingine zinakuwa mbwembwe tu kufanya kazi na wasanii wa nje ili
tutishie wasanii wa ndani kwamba mimi nimeshakuwa mkubwa naweza kukaa
katika nyimbo moja na msanii fulani. Kwa hiyo kama naweza kuwafikia
watu, naweza kutengeneza namba moja 'hits song' bado sina presha
zikitokea sawa sina stress nazo".
Kwa upande mwingine, Mwana
FA amewashauri wasanii wenzake watengeneze nyimbo zilizokuwa bora ili
ziweze kusikilizwa na kila mtu bila ya kubagua mtu wa kusikiliza.
0 comments:
Post a Comment