Pages

Subscribe:

Friday, August 4, 2017

PAM D AWEKA BAYANA TOFAUTI KATI YAKE NA CHEMICAL

Msanii Pam D amekanusha kufanana kimuonekano wa mavazi na Rapa Chemical kwa kuvaa mavazi ya kiume na kudai kwamba katika maisha yake yaliyo nyuma ya umaarufu yeye anavaa kama mtoto wa kike na muonekano wa kiume ni wa kwenye video. 

Pam D ametoa kauli hiyo wakati akimjibu Mtangazaji ya 5Selekt 'Shimii' kutokana na kubadilika kwake katika...
wimbo wake mpya aliomshirikisha Christian Bella kama imetokana na kuchoka mionekano yao ya awali.

"Mimi na Chemical ni watu wawili tofauti, kwa sababu huu ni muonekano wangu wa kibiashara kwenye masha yangu ya kawaida Pam D anaishi maisha ya tofauti kwa kuvaa magauni na kuonekana binti lakini huu muonekano wa vikaptula na wa kiume ni wa biashara kwa sababu mashabiki zangu wanataka niwe hivi na mimi nafanya kile wanachotaka kwa sababu hii ni kazi yangu" Pam D alifunguka.

Pamoja na kupinga kufananishwa kimuonekano na rapa huyo,  Pam D ameongeza katika wasanii ambao anatamani kufanya nao kazi kwa sasa baada ya Bella ni Rapa Chemical.

Akizungumzia kuhusu mahusiano yake aliyokuwa nayo Pam D amedai anakaribia kuwa mke mtarajiwa kwa mpenzi aliyenaye kwa  sasa kwa kuwa amedumu muda mrefu katika mahusiano.
"Story zingine za mtaani zinazosikika juu yangu ni za uongo mimi nina mpenzi ambaye tunatarajia kufunga ndoa ingawa siwezi kumuanika mtandaoni kwani sehemu anayohitajika kujulikana ni kwa wazazi na familia. 

Kwa sasa Pam D anasumbua na ngoma aliyomshirikisha Christian Bella 'Ngoma Droo' aliyoifanya kutoka studio za Free Nation kwa rapa Nay wa Mitego.  

0 comments:

Post a Comment