Msanii Q Chief amemchana swahiba wake wa kipindi kirefu Khaleed Mohamed
'TID' kuwa ana matatizo ya akili na ndiyo maana anazungumza vitu
ambavyo visivyomuhusu kwa jamii.
Q
Chillah amebainisha hayo baada ya kuwepo na ugomvi miongoni mwao hivi
karibuni ambapo TID alihojiwa na EATV kuhusu suala hilo akadai yeye
hamfahamu msanii anayeitwa Q chief na wala hana...
urafiki naye.
“Mimi naona kama watu wazima
kila mtu angeangalia na kupambana na hali yake na kuangalia jinsi gani
anaweza kurudi kwenye nafasi yake ya muziki, Kwa nini kila siku
anizungumzie mimi nahisi kuna kitu special amekiona kwangu na hataki
kuniambia hivyo atakuwa ana matatizo. TID ana matatizo ya kisaikolojia
hivyo anatakiwa ajitathmini kiundani, kama mpaka waheshimiwa wameamua
kumsaidia lazima aonyeshe muelekeo ili waendelee kuwa na imani na
yeye", alisema Q Chillah.
Kwa upande mwingine, Q Chillah amesema hatopenda mambo ambayo ameimba kwenye tungo zake mbalimbali yaje kuwakuta watoto wake. Kwa sasa Q Chief anafanya vyema na wimbo wake mpya 'Naogopa' ambao ameuachia siku za karibuni.



Follow on Instagram
0 comments:
Post a Comment