Msanii wa muziki wa kizazi kipya na mkongwe kwenye game ya bongo fleva Q
Chilla, amesema yeye haitaji kiki ili kazi zake ziweze kufanya vizuri,
tofauti na wasanii wengi wa sasa hivi.
Akizungumza na mwandishi wa habari hii, Q Chilla amesema kazi nzuri inajitangaza yenyewe bila kiki, kwani unaweza ukatengeneza kiki kubwa alafu...
kazi ikawa haina ubora, na kushusha hadhi ya muziki wako.
"Mimi si mtu wa kiki sana kama hivi nianavyosema, lakini i dont know labda nazeeka na heshima za ujana na uzee wangu, lakini naamini kazi inajielezea zaidi kuliko kiki, kwa sababu unaweza ukafanya kiki kubwa halafu kazi ya kawaida, au unaweza ukatoa cover kubwa alafu package ikawa ya kawaida, kwa hiyo ni Mungu tu", alisema Q Chilla
Pia Q Chilla amesema anaamini kazi aliyoitoa leo itafanya vizuri na kumrudisha tena kwenye ramani ya muziki, kwani ni ngoma nzuri ambayo kila mmoja atapenda kusikiliza.
"Mimi nina uhakika kabisa kwa sababu ni ngoma kubwa, ni ngoma ambayo kila mtu angependa kuisikiliza, na niseme nimeitoa kwa kujiamini na naamini ni ngoma kubwa ambayo itazidi kunirudisha, kikubwa ni suport", alisema Q Chilla

0 comments:
Post a Comment