Ikiwa imebakia siku kuelekea mtanange kwa mechi ya Ngao ya Jamii, rapa
Roma Mkatoliki ambaye ni mshabiki namba moja wa klabu ya Simba
amefunguka akidai siku hiyo atakuwepo uwanja wa Taifa kwa lengo la
kuwapa hamasa wachezaji na mashabiki wa Simba.
Roma
amebainisha hayo muda mchache alipotoka katika kipindi cha Planet Bongo
ya East Africa Radio na kusema siku hiyo timu ya Yanga ijiandae kwa...
kupokea kichapo kitakatifu.
"Wanangu wote mashabiki wa
timu ya Simba tukutane Taifa kwa ajili ya kumng'oa huyu jamaa wa rangi
ya njano (Yanga), tutamkalisha Stamina na wanae wote wanaoshabikia timu
hiyo. Najua mashabiki wa Yanga hawataamini kitakachotokea sisi hatuongei
sana",alisema Roma.
Katika hatua nyingine, msanii Stamina
ambaye ni shabiki wa Yanga amedai timu hiyo haina upinzani na klabu
yoyote kwa kuwa timu ya Yanga ndiyo imeshikilia rekodi ya ushindi mpaka
sasa.
0 comments:
Post a Comment