Pages

Subscribe:

Friday, August 11, 2017

UKARIBU WA YVONNE CHAKACHAKA NA JOKATE WAZUA MASWALI


UKARIBU uliojitokeza hivi karibuni kati ya mwanamitindo, Jokate Mwegelo na mkongwe wa muziki kutoka Afrika Kusini, Yvonne Chakachaka umeibua maswali mengi huku wengi wakihoji kulikoni.

Kwa mujibu wa chanzo, Jokate ambaye yupo nchini Afrika Kusini kwa shughuli binafsi, amekuwa akionekana mara kwa mara kuwa karibu na Chakachaka na kufikia hatua ya...
kufurahia kukutana na mama aliyekuwa akimtafuta kwa muda mrefu.

“Jojo (Jokate) ana furaha sana kukutana na Chakachaka na muda wote amekuwa akimuita mama… mama, si unakumbuka mwanzoni Ali Kiba naye alishawahi kukutana na Chakachaka wakarekodi na wimbo kisha akaandika katika kurasa zake katika mitandao ya kijamii kwamba anamshukuru mama (Yvonne) kwa kila kitu anachomfanyia.
Alikiba na Yvonne Chakachaka.

0 comments:

Post a Comment