Mwanamuziki
Ali Salehe Kiba amepangua tuhuma za kuiba wimbo unaosumbua kwa sasa
mtaani 'Seduce Me ' na kusema kuwa katu kitu kama hicho hakitaweza
kikatokea kwenye maisha yake na kuwatoa hofu mashabiki zake wasiumizwe
na maneno kwani anajiamini.
Alikiba
amelazimika kupangua tuhuma hizo baada ya kuwepo na maneno mitandaoni
ya kwamba wimbo wa 'Seduce Me' uliotengenezewa na mtayarishaji Man Water
umfanyiwa 'copy' kutoka...
kwenye wimbo ulioimbwa na kwa lafudhi ya
kiharabu .
"Siyo kweli kama nimeiba
wimbo. Hicho ni kitu ambacho sijawahi kufanya na hakitaweza kutokea
kwenye maisha yangu yote kwa sababu najiamini. Nawaomba mashabiki zangu
waendelee kufurahia muziki mzuri. Duniani kote nyimbo ambazo zimefanya
vizuri zimetengenezewa 'cover' nyingi sana, hivyo ndivyo ilivyotokea
kwenye wimbo wangu kwahiyo nawasihi mashabiki zangu wasiogope kwa
kudhani nimeiba wimbo wa mtu" alisema Alikiba.
Pamoja na hayo Alikiba
amewasihi mashabiki zake wasiwe na hofu kwani hawezi kukaa kimya kwa
muda mrefu kwani mwaka huu amepanga kuwafurahisha na pindi watakapokuwa
wanataka ngoma mpya wasisite kumtaarifu ili aachie kazi nyingine mpya.
Kwa sasa Alikiba
anasumbua na ngoma inayokwenda kwa jina la 'Seduce Me' iliyotoka Agosti
25 ambapo mpaka sasa inawatazamaji zaidi ya milioni 4 katika mtandao wa
YouTube kupitia account yake ya 'Vevo'.
0 comments:
Post a Comment