Pages

Subscribe:

Monday, October 9, 2017

AKON AMKINGIA KIFUA NELLY JUU YA TUHUMA ZA KUBAKA


Baada ya kukumbwa na janga la kutuhumiwa kufanya Ubakaji siku ya jumamosi katika Tour bus ambayo huitumia katika ziara zake huko washington, Nelly aliamua kufunguka kwa mara ya kwanza kwenye kurasa yake ya Twitter kwa kusema kwamba hilo kosa amesingiziwa na nia nikulichafua jina lake.

Kupitia mfululizo wa Tweets zake ambazo anawashukuru mashabiki wake kwa kuwa nae Bega kwa bega na kumuamini kwamba...
hajafanya tukio hilo, Sasa Moja ya washikaji wake wa karibu, Akon ameamua kuongezea kwamba anamfahamu Nelly Muda mrefu na hadhani kama Nelly anaweza kufanya jambo kama hilo.

Baada ya #nelly kumake headline kwa shutuma za Ubakaji akiwa kwenye Tour bus lake huko Washington, Mshikaji na msanii mwenzake, #akon ameamua kufunguka juu ya sakata hilo kwa kudai kwamba Nelly hawezi fanya kitu kama hicho. #officialsocialbuzz 

Kupitia video ambayo imepostiwa na mtandao wa Tmz inamwonyesha Akon akifunguka na kutoa maoni yake kuhusu Ishu hiyo ambayo imemgusa kila mtu na kumake headline kwa tukio hilo la Nelly.

0 comments:

Post a Comment