Pages

Subscribe:

Monday, October 9, 2017

DIAMOND PLATNUMZ ATIKISA UK NA HALLELUJAH


"she said she want some more, harder  than i gave her before"....Dallas Texas see you On the @afrimma Awards tonight!!! #hallelujah Video link in my BIO...

Diamond Platnumz haishi kutuamsha na habari kubwa zinazohusiana na nyimbo zake kila kukicha.

Baada ya kuachia wimbo wake mpya ‘Hallelujah’ ambao amewashirikisha Morgan Heritage kuweka rekodi kubwa ya kufikisha views milioni moja ndani ya masaa 15, wimbo huo umeonekana kufanya vizuri katika kituo cha BBC Radio 1Xtra ya...
nchini Uingereza.

‘Hallelujah’ umeshika namba moja katika Top 5 ya kipindi cha Afro Boss cha radio hiyo kwa kuzishinda ngoma nyingine kama ‘Inde’ ya Heavy K, ‘Maradona’ ya Niniola, ‘My Baby’ ya Magnom na ‘Nhema’ ya EXQ .

Wimbo huo unaendelea kufanya vizuri nchini humo ikiwemo na kwenye kituo kingine cha Capital Xtra.

0 comments:

Post a Comment