Msanii wa muziki wa bongo fleva Msami ambaye kwa sasa anafanya vyema na wimbo wake mpya 'Mabawa' amefunguka na kusema ni kweli alikuwa anatoka kimapenzi na Irene Uwoya lakini toka wameachana wamebaki kuwa marafiki na hawana tatizo lolote lile.
Msanii akiwa kwenye kipindi cha Planet bongo amedai kuwa hata alipokuwa akitoka na Irene alikuwa hana tabia ya kumfuatilia katika mambo yake ayafanyayo ila amedai licha ya...
kuwa mahusiano yao yalikufa lakini wamekuwa wakiwasiliana kama kawaida.
"Ndiyo ni kweli nilikuwa natoka na Irene Uwoya lakini katika kipindi chote hicho sikuwahi kumfuatilia katika mambo yake alikuwa huru kabisa, japo tumeachana lakini mimi na yeye tupo sawa kabisa kwani mawasiliano yapo kati yetu" alisema Msami.
Pia msanii huyo amedai kuwa yeye aliamua kujiweka tofauti na baadhi ya 'Dancers' ambao wanafanya kazi na wasanii mbalimbali ili tu akuze thamani yake katika kazi yake hiyo.
"Unajua mimi nilifanya kwa muda kuwa chini ya msanii fulani lakini nikaamua kujiweka tofauti ili niweze kujiongeza thamani yangu, kama hivi msanii yoyote ambaye atahitaji mimi kumsaidia jambo fulani kuhusiana na kazi yangu ya kucheza anakuwa anatambua thamani yangu katika jambo hilo" alisema Msami.
0 comments:
Post a Comment