Pages

Subscribe:

Monday, August 14, 2017

BARNABA: KUMTUKANA MWANAMKE NI SAWA NA KUMTUKANA MAMA

Mwanamuziki anayesumbua kwa sasa na ngoma ya 'Tunafanana' Barnaba Elias 'Barnaba Classic' ametupa jiwe gizani linalodaiwa kuwa ni dongo kwa mzazi mwenzake baada ya kufunguka kwenye mtandao kuwa kumtukana mwanamke ni sawa na kumtukana mzazi wake. 

Dongo hilo Barnaba ameliweka kwenye ukurasa wake wa Instagram baada ya mzazi mwenzake huyo kudai kuwa baada ya miaka mtano kupita hatimaye sasa amefanikiwa kupata...
amani ya moyo ambayo ndicho kitu alichokuwa akikikosa kwa muda wote.

Barnaba ameandika "Mama aliniambia ukimtukana mwanamke basi umenitukana na mimi. Siku zote nawaona kama mama zangu hongera wanawake wote duniani Salamu zangu juu yenu Jumapili ya leo nawapenda Sana"


Ujumbe wa Barnaba aliouweka Instagram jana baada ya ujumbe wa Mzazi mwenzake Mzazi mwenzake Barnaba, Zuu Namela ambaye walibahatika kupata mtoto wa kiume 'Steve' jana asubuhi aliandika kwenye ukurasa wake wa Instagram kisha kufuta ujumbe huu.

"Ni watu wachache sana wanaojua nikitu gani nilikua nakosa katika maisha yangu! Unaweza ukapata kila kitu kwenye maisha ila ukakosa furaha,amani,heshima......kwa zaidi ya miaka mitano hichi ndo nilicho kuwa nakitafuta #AMANIYAMOYO " 

Ujumbe wa mzazi mwenzake Barnaba, Bi Zuu Namela kabla ya kuufuta.

0 comments:

Post a Comment