Msanii Zuwena Mohamed Shilole' amekanusha kauli yake ya kushindwa
kuachia ngoma kwa kipindi cha miezi mitano kutokana na kudukuliwa kwa
mtandao wake wa (Instagram) na badala yake alikuwa akiusoma mchezo huku
akisubiria majibu ya ngoma 'Hatutoi Kiki.
Shilole
amedai kuwa watu wanaozungumza kwamba yeye amekaa kimya muda mrefu ni
kutokana na wengi wao kumiss kuona...
vituko na tashtiti zake katika
mitandao ya kijamii hivyo hata wakati akiwa amejiandaa kutoa wimbo mpya
bado alionekana kama kapooza.
"Siyo kweli kama nategemea
Instagram kutoa kazi, kwani bila hiyo Insta zamani watu walikuwa
wanafanyaje? Sijatoa wimbo kwa sababu nilitaka wimbo wa 'hatutoi kiki
uendelee kusogea na siyo kwamba kwa sababu nilikuwa sina mtandao wa
Instagram ndiyo nikaamua nitulie. Lakini kwa sababu najua kuna
wasiosikiliza radio na na wasiotazama Tv ndiyo maana pia nilitulia
kuusoma mchezo kwa kuwa nilitaka niwapate wote na mashabiki mashabiki wa
mtandaoni ndiyo maana nilichelewa kidogo" Shishi alifunguka.
Hata hivyo Shilole ameongeza kuwa "mashabiki
waliopokea wimbo wangu huu ndiyo mashabiki wa kweli siyo wale
wanaosubiri tashititi za kukaa uchi au kelele zangu ila" Shilole.



Follow on Instagram
0 comments:
Post a Comment