Msanii wa muziki wa kizazi kipya asiyeisha vituko Shilole amemtetea
mwanaume wake mpya baada ya tuhuma za kutoka na serengeti boys.
Akizungumza kwenye kipindi cha Planet Bongo cha East Africa Radio, Shilole amesema kwa sasa yeye hana mahusiano na wanaume ambao amewazidi umri, kwani mpenzi wake wa sasa ni mwanaume halisi (gentle man) na amemfanya...
awe na mawazo ya kuwa mke.
Hata hivyo Shilole ambaye leo ameachia wimbo wake mpya unaoitwa
'Kigori', amewatetea watu ambao wana mahusiano na wanaume wanaowazidi
umri (serengeti boys) na kusema siyo kitu cha ajabu kwani umri ni namba
tu, kinachomata ni mapenzi.
Hapo nyuma Shilole alishawahi kukumbwa na sakata la kuwa na mahusiano
na wanaume wenye umri mdogo (serengeti boys) akiwemo aliyekuwa mpenzi
wake Nuhu Mziwanda.
Akizungumza kwenye kipindi cha Planet Bongo cha East Africa Radio, Shilole amesema kwa sasa yeye hana mahusiano na wanaume ambao amewazidi umri, kwani mpenzi wake wa sasa ni mwanaume halisi (gentle man) na amemfanya...
awe na mawazo ya kuwa mke.
"Mwanaume wangu wa sasa sio
serengeti boys, ni gentle man, anajielewa na pia ni mtu mzima,
ananifanya mpaka nifikirie kuolewa niwe mke, yaani sio serengeti boy
kabisa, na pia hataki kabisa mambo ya mitandao na ndio maana simuweki
wazi", alisema Shilole.
"Kwani kitu gani...!! age is just a number, watu wanaangalia mapenzi bwana so its not a big deal kuwa na kiserengeti", alisema Shilole.
0 comments:
Post a Comment