Pages

Subscribe:

Wednesday, March 22, 2017

ASKOFU GWAJIMA KUTEMBELEA OFISI ZA CLOUDS FM SIKU YA LEO

Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Bishop Josephat Gwajima amesema kuwa Jumatano hii atatembelea Clouds Media Group kwajili ya kuwapa pole kwa yaliyotokea hivi karibuni.

Ijumaa iliyopita kituo hicho kilivamiwa na Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda akiwa na askari wenye mitutu  kuvamia Ofisi za Clouds Media Group, kwa lengo la kushinikiza...
habari yake irushwe katika kipindi cha Da’ Weekend Chat Show maarufu kama (Shilawadu) kitendo kilichopingwa na wadau mbalimbali wa habari.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Gwajima ameandika “Kesho Tarehe 22/03/2017 saa nne kamili asubuhi, nitatembelea Ofisi za Clouds Media ili kuwapa pole kwa yaliyotokea.”

0 comments:

Post a Comment