Mwanamitindo maarufu nchini Hispania,
Georgina Rodriquez ambaye ni mchumba wa mshambuliaji wa Real Madrid na
timu ya Taifa ya Ureno, Cristiano Ronaldo, anatarajia kujifungua watoto
mapacha.
Kwa mujibu wa Gazeti la The Sun
limeripoti kuwa, mchezaji huyo ameweka wazi kwamba ameandaa nyumba yenye
thamani ya Sh bilioni 13 kwa ajili ya kufikia watoto hao na pia ameweka...
vito mbalimbali vya thamani kwa ajili yao.
Ronaldo ambaye kwa sasa ana mtoto mmoja
wa kiume anayejulikana kwa jina la Cristiano Jr, ujio wa watoto hao
utaongeza ukubwa wa familia yake lakini kwa mchumba wake huyo mwenye
umri wa miaka 23 itakuwa ndio watoto wake wa kwanza.
Kupitia akaunti ya Instagram, Georgina
amedai kuwa familia hiyo kwa sasa ipo katika furaha kubwa ikiwa
inatarajia kupata watoto hao wawili. “Muda mfupi ujao familia itakuwa kubwa na Cristiano Jr. anatarajia wadogo zake wawili, tuna furaha mno,” aliandika Georgina.
0 comments:
Post a Comment