Pages

Subscribe:

Thursday, March 16, 2017

FAIZA ALLY ASHINDWA KUZUIA HISIA ZAKE KWA ALIKIBA

Aliyekuwa mke wa Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ ambaye pia ni msanii wa filamu na Mama wa mtoto mmoja, Faiza Ally ameamua kuweka wazi hisia zake kwa msanii wa Bongo Fleva Ali Kiba. Yaani kama ingekuwa ni mahaba basi tunasema mahaba mubashara kwani sio kwa kumsifia kule!!

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Faiza amefunguka kuwa usiku wa kuamkia leo amemuwaza Ali Kiba na kusikiliza nyimbo zake na kuongeza kuwa ni kijana mzuri sana na...
kuweka emoji ya maua ya upendo (Kopa).

“Nimeamka namuwaza tu nasikiliza nyimbo zake huyu kijana mzuri bwana dah hlf Ana class flan hivi yaani wajanja tu kama mm ndio tuna muelewa “Ameandika Faiza Ally Instagram.

0 comments:

Post a Comment