Msanii Fid Q amesema anashangazwa na
baadhi ya watu wanaomuandika vibaya katika mitandao ya kijamii kuwa ana
‘bifu’ na Joh Makini kutoka Weusi hali ya kwamba hawana tofauti yoyote
baina yao. Kubanda alifunguka zaidi kwa kusema
hajawahi hata kuwaza kugombana na ‘rappa’ huyo mwenye ‘hit song’
inayojulikana kwa jina la waya.
“Unajua hata mimi nilikuwa
nazipokea tu hizo ‘story’ kama wanavyopokea watu wengine maana sijawahi
kuwa na shida na jamaa, kawaida ya wabongo huwa tunatafuta...
‘challenger’
kama mtu mpya akiingia kwenye game so Joh alitumiwa kama ‘challenger’
wangu maana mimi nafanya vizuri tangu back then”. Alisema Fid Q.
Mbali na hilo mkali huyo amesema njia ya
muziki na kibinadamu hana kinyongo wala ugomvi pia aliendelea
kusisitizia kuwa yeye ndiye aliyemuunganisha Joh katika ‘project’ ya nje kwenda kufanya kazi japokuwa muhusika mwenyewe atakuwa hatambui hilo.
0 comments:
Post a Comment