Pages

Subscribe:

Monday, March 6, 2017

FID Q AFUNGUKA KUHUSU UJIO WAKE WA ALBUM YA TATU


Imekuwa kama mazoea hivi kwamba kila ifikapo tarehe 13 ya mwezi August basi ni lazima tupate kitu kipya kutoka kwa rapper Fid Q. Kwasababu ni tarehe ambayo anaadhimisha siku yake ya kuzaliwa na yeye kupenda kuwapa zawadi mashabiki zake tofauti na watu wengine ambao hupenda kupewa zawadi siku kama hiyo.

Kwa kumbukumbu ya miaka hii miwili, mwaka jana 2016 August 13 Fid Q alidropisha ngoma ya SUMU, huku mwaka juzi 2015 mkali huyo aliachia Kemosabe.
Round hii mkali huyo amepania kufanya...
kibabe zaidi kwa kudondosha Album nzima ambayo kaipachika jina la Kitaolojia.

Ni kwenye The Playlist ya Times FM ndipo ambapo Fid Q alialikwa weekend iliyopita na kuweza kuzungumzia mengi zaidi kuhusiana na mchongo huo.

Baadhi ya maneno ambayo nilimnukuu Fid Q akifunguka kuhusiana na  album hiyo ni pamoja na “Gud News kwa fans na wanafamilia wote wa Fid Q ni kwamba August 13 inakuja Kitaolojia ambayo ni Album yangu ya 3, kumbuka kwamba nina album mbili tayari, yakwanza ni Vina mwanzo, kati na mwisho, ya pili ni  Propaganda, sasa nafanyia kazi album yangu ya tatu ambayo nimeipa jina la Kitaolojia.”

0 comments:

Post a Comment