Msanii G Nako kutoka 'Weusi' amewataka wasanii na watu wanaohitaji
kuwekeza na kufanya biashara ya muziki wasiogope changamoto zilizomo,
bali fursa na uwezo wao wa kuzikabili, huku akiwakosoa wanaweka
changamoto hizo hadharani.
G
Nako amesema kwenye kila
kazi kuna changamoto nyingi lakini kuziongelea kwenye vyombo vya habari
ni kuwakatisha tamaa wale wachanga wanaotaka kuinuka na kuwazuia
kuonesha...
uwezo wao.
“Hakuna kazi isyokuwa na
changamoto lakini kuzisema hadharani ni kuwakatisha tamaa wasanii
wachanga wanaotamani kufanya kama mimi au wanaonitazama mimi,mimi
nawashauri kama kuna mtu anapenda kufanya hii biashara au kuwekeza
kwenye muziki asisikilize maneno ya watu kwa sababu yatakukatisha tamaa
ya kujaribu” - Gnako
Katika hatua nyingine G Nako
amesema muziki anaoufanya ni muziki wa ukombozi hivyo kila mtu huwa
anawasilisha mawazo kwa mtindo ambao ana uwezo nao na kusisitiza kuwa
ukombozi unadaiwa siyo kuombwa. Aidha ameongeza kuwa kundi lake la Nako 2
Nako bado lipo halijavunjika kama jinsi wengi wanayofikiria na
tayari wana nyimbo zisizopungua tano zinasubiri kuachiwa.
"Nako 2 nako tupo hata kazi
tulizofanya nazo zipo, tuna kazi kama sita tumeshatengeneza hapa
ikitokea project tunaweza kufanya albam, tatizo linakuja tu kwamba mimi
nafanya 'movement' zangu kivyangu na wenzangu vivyo hivyo, muziki ni
biashara mwisho wa siku studio unalipa, matangazo na mengineyo
kusipokuwa na usimamizi ni hasara,sisi bado hatujapata mtu wa kusimamia
kazi”. G Nako
0 comments:
Post a Comment