Pages

Subscribe:

Thursday, March 9, 2017

HARMORAPA ANATARAJIA KUSHANGAZA WENGI 2017


Alianza kama utani hivi kwa kufananishwa na mkali wa lebo ya WCB then mdogo mdogo anaanza kupenya kwenye masikio ya wapenda burudani.

Hapa Tunamzungumzia HarmoRapa Jamaa anatabiriwa kufanya makubwa kwenye mziki wa bongo fleva Time hii hapa. Single yake ya kwanza usigawe pasi ndiyo iliyomuweka kwenye ramani na kuanza...
kujulikana japo haikufanya vizuri sokoni.
 
This Time around HarmoRapa amekuja na another hit in Town goes by the name “Kiboko ya Mabishoo” wengi walidhani kama ni Jokes lakini Jamaa amekuwa serious sasa baada ya kusaini deal na kampuni kubwa ya upigaji picha na teknolojia bongo Slides Visual chini ya Mx Carter.

Jamaa kwa kasi hii anatabiriwa kusumbua kwenye game wasanii waliopo hawatakiwi kubweteka na kasi hii ya ukuaji wa ajabu na  wanatakiwa wamuangalie zaidi sababu yupo chini ya  menejimenti nzuri inayofanya promotion ya uhakika kuendana na soko la sasa.

kupitia mitandao ya kijamii Facebook, Twitter na Instagram jina  la Harmorappa limezungumzwa Mara nyingi na Story zake zikifuatiliwa kwa wingi na wapenzi wa burudani Bongo.

0 comments:

Post a Comment