Hayo yamekuja baada ya msanii huyo kuombwa pesa ya mavazi na Juma
Nature kwaajili ya kufanyia ‘shooting video’ jambo ambalo kwa upande
wake limemkwaza kwa namna moja ama nyingine. “Haipo sawa kwa wasanii wakubwa
kutudai sisi ‘underground’ pesa ya kufanyia collabo wakati...
wanajua bado
hata hatuanza kufaidika na muziki wenyewe”. Alisema Harmorapa kwenye kipindi cha eNewz ya EATV.
Aidha Harmorapa amesema muda mwingine
wasanii wakubwa wanatumia njia ya kutaka pesa ndefu ili mradi wa
kwamishe kufanya kazi nao.
Kwa upande mwingine mzee wa kiki za mjini
amesema mashairi aliyoyatumia katika wimbo wake amefanya kumjibu
‘dansa’ Mose Iyobo kutoka WCB kwa kile alichokifanya awali cha
kumfananisha na sokwe.
0 comments:
Post a Comment