Pages

Subscribe:

Monday, March 6, 2017

JACQUELINE WOLPER: SASA INATOSHA ACHENI KUMTUKANA MAKONDA



Muigizaji wa filamu nchini, Jacqueline Wolper amemkingia kifua mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, akiwataka watu kuacha kumwandama kwa kashfa yake ya kufoji vyeti pamoja na kumtukana mtandaoni.

Kwa wiki kadhaa sasa, Makonda amekuwa akiandamwa mtandaoni kutokana na tuhuma kuwa jina analotumia si lake, na kwamba lake ni Daudi Bashite. Jumapili hii kumesambaa video mtandaoni ikimuonesha...
mkuu huyo wa mkoa akilia kwa uchungu kanisani baada ya kuzungumza na mchungaji akimbembeleza.

“Nimevaa kiatu chake kimenibana mpaka kinataka kunipasua kisigino,” ameandika Wolper kwenye Instagram.

“Jamani wa Tanzania tuwe na utu, acheni kumtukana huyu kaka daaaah hivi ni nani ambae yupo perfect mpk aanze kumtukana kaka wa watu jmn. Nimepost nikiwa km binadam wa kawaida ambae nina moyo!muhurumieni kaka watu acheni Mungu awe muhukumu basi,” ameongeza.

0 comments:

Post a Comment