Msanii mkongwe anayetamba na ngoma ya ‘Nisaidie Kushare’, Juma Mchopanga ‘Jay Moe’ maarufu zaidi kama ‘Famous’ amekanusha kumchana Izzo Biznez katika ngoma hiyo na kwamba Izzo mtu wake karibu ambaye wanashirikiana kwenye kazi nyingi.
Jay Moe alisema watu wametafsiri vibaya
kwa kumuhusisha Izzo na wimbo huo pia kumuweka kwenye kundi la wasiojua
ni kosa , na kuongeza kuwa yeye amewachana...
watu wote ambao wanafanya
kazi mbaya na kusumbua watu kuwasaidia kuweka picha za kazi zao katika
mitandao ya kijamii.
Majibu hayo yamekuja baada ya tetesi
zilizopo mitaani ya kwamba katika wasanii wanaoongoza kwa kuomba watu
waweke matangazo ya nyimbo zake kwenye mitandao lakini akitoa nyimbo
zinabuma kwa kuwa hawekezi kwenye kuangalia kuandika nyimbo bali picha.



Follow on Instagram
0 comments:
Post a Comment