Pages

Subscribe:

Thursday, March 16, 2017

KAULI YA MWANASHERIA WA DONALD TRUM JUU YA SNOOP DOGG


Mwanasheria wa Donald Trump amjia juu Snoop Dogg kufuatia video yake mpya ya ‘Lavender’ akiwa anamwonyeshea bastola Donald Klum, Donald Trump wa uwongo ambae ametumika ndani ya video hiyo.

Kupitia mazungumzoyake aliyoyafanya na mtandao wa TMZ, Mwanasheria huyo wa Trump,  Michael Cohen alifnguka kwa kusema kwamba kitendo ambacho amekifanya Snoop Dogg ni udhalilishaji...
kwa Rais Donald Trump na kusema kwamba Snoop anapaswa kuomba msamaha kwa kitendo chake.

Ni sawa kufanya utani lakini kwa upande wa Snoop Dogg amevuka mipaka ya utani kwa kile kikubwa ambacho alikifanya cha kutoa pisto ya uongo na kuinyoosha kwa mfano huo wa Donald Trump huku ikiwa imeandikwa ‘Banng’, Cohen anasema kwamba hakuna utani wa mauaji kwa Rais na kitendo hiko kimemshtua sana mwanasheria huyo wa Trump.

“Nisingeweza kulikubali jambo hlo hata kama Raisi angekuwa ni Barack Obama, na vilevile siwezi kukubali hata kwa Donald Trump, unajua kitu ambacho kinanisikitisha kwa Snoop Dogg ni kwamba kuna vitu vingi sana ambavyo angeweza kuvifanya kwa jamii lakini sio kwa video hii” aliongea Michael Cohen.

0 comments:

Post a Comment