Balozi wa Hungary hapa nchini mwenye makazi yake Nairobi, Kenya Mhe.
Lazaro Eduard Mathe amemhakikishia Rais wa Tanzania Dkt. John Magufuli
kuwa nchi yake ipo tayari kushirikiana na Tanzania katika kuendeleza
sekta ya viwanda
Pia Balozi huyo amemuhakikishia kwamba wawekezaji kutoka Hungary
wameanza kufanya mchakato wa kujenga kiwanda cha kuunda mabasi ya...
abiria.
Mhe. Lazaro Eduard Mathe amesema hayo leo Ikulu Jijini Dar es Salaam,
wakati akizungumza na Mhe. Rais Magufuli muda mfupi baada ya kukabidhi
hati zake za utambulisho akiwa ni miongoni mwa Mabalozi sita
waliokabidhi hati hizo.
Pamoja na nia ya kujenga kiwanda cha kuunda mabasi ya abiria, Mhe.
Lazaro Eduard Mathe amempongeza Mhe. Rais Magufuli kwa juhudi kubwa
anazofanya kujenga uchumi wa Tanzania na ameahidi kuwa Hungary itakuza
na kuimarisha ushirikiano wake na Tanzania kwa kuleta teknolojia katika
sekta mbalimbali ikiwemo viwanda na kilimo pamoja na kuwahimiza
wawekezaji kuja kuwekeza nchini Tanzania.
0 comments:
Post a Comment