Ktk mahusiano kuna mambo mengi ambayo yanapelekea watu kuachana ila kuna kasoro 6 amazo mwanaume ukiwa nazo basi wanawake lazima watakukwepa. Nimekuwekea kuanzia moja mpaka sita uzisome hapa.
1. Wakikosa attention yako. Wasichana hupenda pale wanapofahamu kuwa
unawasikiliza na unafahamu nini wao wanahitaji. Kama kutakosekana
mawasiliano mazuri na atagundua hilo atauona uhusiano huo... haumtimilizii
haja zake. Hata kama kila kitu kinaenda sawa. Msikilize anapoongea. Kama
akiona hapati penzi analolihitaji atatafuta mwingine ambaye yupo tayari
kumtimizia.
2. Kumuheshimu. Msichana huwa anajitoa sana awapo katika mahusiano hivyo
anategemea mvulana uheshimu hata kwa chochote kidogo anachokufanyia.
Mfanye agundue kuwa umeheshimu kile ambacho amekufanyia.
3. Usaliti. Unaposaliti inamaanisha kuna kitu hakipo sawa katika
mahusiano yako hata kama una uwezo wa kushughulikia lakini wewe unaona
njia sahihi ni kutoka nje kuwa na mahusiano na msichana mwingine
ukidhani ndio unarekebisha. Pale msichana wako akikukamata unamsaliti
fahamu hawezi kuvumilia naye atakuacha.
4. Ukosefu wa hisia za kimapenzi. Msichana hupenda kuona kuwa wanapendwa
wanathaminwa na wapenzi wao wanawajali sasa wakiona kuwa hakuna
conection ya hisia za kimapenzi kutoka kwa mvulana wake huona kuwa
hakuna mapenzi ya kweli katika uhusiano aliopo
5. Hawapendi kusikia kuhusu mapenzi mara kwa mara wasichana hupenda
kutumia muda mrefu na wapenzi wao bila kusikia neno la kuwataka wafanye
mapenzi kama ukiwa nao na ukawataka kimapenzi mara kwa mara watakuwa
wanakuavoid hata utakapokuwa ukiwagusa.
6. Unapomcontrol sana
msichana humpenda mvulana atakayemlinda na kujiona yupo sehemu salama sio kumdhibiti kufanya mambo yake mengine anapenda uhuru.
0 comments:
Post a Comment