Mwanafunzi wa Shule ya Msingi Ruwenzera amedai kufanya ngono na walimu
wake watatu kwa nyakati tofauti baada ya kuahidiwa kupewa zawadi na
fedha.
Akizungumzia sakaa hilo, mwenyekiti wa kamati ya shule hiyo, Masele
Omary alisema kuwa Machi 7 uongozi ulikutana na kufikia uamuzi wa
kumuomba mkurugenzi mtendaji wa wilaya awaondoe walimu hao baada ya...
kujiridhisha na maelezo yaliyotolewa na mwanafunzi huyo.
Kwa mujibu wa mwanafunzi huyo anayesoma darasa la saba, alifanya ngono
na walimu hao kwa nyakati tofauti baada ya kumshawishi kumpa Sh10,000 na
mwingine kuahidi kumnunulia nguo za ndani.
Alidai mwalimu Gerard Paulo alimuahidi kumnunulia nguo za ndani, huku
Osner Yohana na mwingine (jina linahifadhiwa kwa kuwa hakupatikana
kuzungumza) alimshawishi kwa kumpa Sh10,000 kila mmoja.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti, Paulo na Yohana walikana kumrubuni
mwanafunzi huyo wakidai tuhuma hizo zinatokana na wao kuhoji matumizi ya
fedha za ukarabati na michango ya chakula.
0 comments:
Post a Comment