Wednesday, March 22, 2017
OMMY DIMPOZ ATOA SABABU YA WIMBO WA KAJIANDAE KUKAA KWENYE YOUTUBE CHANEL YA ALIKIBA
Moja kati ya mambo ambayo yalikuwa yakiwachanganya watu wengi ni pamoja na kitendo cha video ya wimbo wa Kajiandae kukaa kwenye Youtube Chanel ya Alikiba wakati wengi walitambua kwamba wimbo huo unamilikiwa kwa asilimia kubwa na Ommy Dimpoz.
Ommy Dimpoz amefunguka kuwa ile ngoma ni collabo na sio featuring, na kuhusu video kukaa kwenye chanel ya Alikiba hiyo ilikuwa ni makubaliano yao na wala haijaathiri kitu chochote kwasababu makubaliano yao ni...
kugawana asilimia 50 kwa kila mmoja.
Na hivyo video hiyo iliwekwa katika chanel ya Alikiba ili kutaka trafic kubwa ya watu kuitazama kwasababu chanel hiyo ilikuwa na subscribers wengi kuliko chanel ya Ommy Dimpoz.
Nimekuwekea interview hiyo wakati Ommy Dimpoz akifunguka hayo kwenye video hii hapa chini, unaweza kusikiliza kwa kubonyeza play kwenye video hii hapa chini.
Labels:
HABARI & UDAKU
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment