Mkongwe wa bongo fleva kwenye mahadhi ya
hip hop, Prof Jay wa Mitulinga jana amedropisha ngoma yake mpya
inayokwenda kwa jina la ‘Kibabe‘ ambao ni hiphop
iliyozoeleka kutoka kwake baada ya kukaa mda mrefu tangu atoe wimbo
wenye mahadhi ya hip hop singeli ulioitwa ‘Kazi kazi’
Prof. Jay ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo
la Mikumi amesema nyimbo za kiharakati zilimpelekea kuwa Mbunge kabla ya
kuingia Bungeni kwa kuwa kila wimbo ambao aliokuwa anaufanya ulikuwa
unabeba...
shida za wananchi kiuhalisia na kuendelea kusema kuwa hawezi
kubadilika.
Mbali na hilo Prof Jay amewataka wasanii
wa singeli kukomaa katika muziki huo ili waweze kuufikisha mbali na
siyo kubweteka kusubiri watu wengine kuwanyanyua ili waonekane. Alidai
yeye hana mpango wa kuendelea kuimba muziki huo na kwamba alijitoa
kufanya wimbo mmoja ili kuonesha vipaji vilivyopo kwenye muziki huo
ikiwa ni pamoja na kuupa hadhi kwenye jamii.
“Mimi napenda kusapoti vipaji
vilivyopo mitaani, hata leo ukinipa jezi nicheze mpira ili kuhamasisha
watu waupende mpira nitacheza lakini siyo sehemu yangu, kuhusu Singeli
mimi siwezi tena kuimba nilivyoimba ule wimbo nilitaka kuonesha jamii
kuwa kuna muziki huu pia upeni ushirikiano, sasa wasanii wenye wimbo huo
ndiyo wenye jukumu la kuhakikisha unakua, Mwaka huu wameonekana kupooza
wanatakiwa wapambane” Jay alisisitiza ndani ya Planet Bongo.
0 comments:
Post a Comment