limekuwa
suala zito kwa wasanii wengi wanaosign na label kubwa za Marekani mara
nyingi huishia kupotea kwenye game, na Tiwa Savage ni miongoni mwa
wasanii waliohofiwa kutokewa kwa jambo hilo baada ya kusign mkataba na
Roc Nation label ya Jay Z.
Kwa mujibu
wa ripoti ya Urban View ya Nigeria, mwaka jana, Jay Z alishawishiwa na
uwezo wa Tiwa na alikubali kumsign mnamo May 24 mwaka jana. Ilidaiwa
kuwa deal lilisimamiwa na...
wawakilishi wa Roc Nation, Briant Biggs na
Shawn Pecas. Tiwa Savage ndiye msanii wa kwanza kutoka Nigeria
kusainishwa kwenye label hiyo na alijiunga na Rihanna, Big Sean, DJ
Khaled na wengine.
Jay Z, Tiwa Savage & Don Jazzy
Katika Interview ya hivi karibuni na NotJustOK TV ya Nigeria. Tiwa alifunguka vitu vingi vya maisha yake ya sasa ikiwemo pia maisha yake ya kimuziki toka ajiunge na Roc Nation.
Moja ya vitu
alivyoviweka sawa ni pamoja na kunyoosha maelezo juu ya madai
yaliyowahi kutolewa na wadau baada ya kujiunga na label hiyo kubwa
kutoka Marekani, madai hayo yalisema “Roc Nation inamlazimisha
kubadilisha aina ya muziki anaoufanya” ambapo alisema..
“Ninachokipenda
kuhusu kukutana na kukaa na Jay Z ni alituambia mimi na Jazzy kuwa
hataki nibadilike, alinizuia kabisa. Alisema kwa msisitizo kuwa
kilichomvutia kuhusu mimi na brand yangu ni kile nilichokuwa nakifanya”
Mbali na hilo, Tiwa Savage pia alichukua time na kuweka sawa kuwa bado yupo Mavin Records na Don Jazzy
“Nimesigniwa Roc Nation, nina mkataba wa kuwa- managed huko lakini label niliyopo ambayo ni familia yangu bado ni Mavin Records“
0 comments:
Post a Comment