Pages

Subscribe:

Wednesday, October 4, 2017

GIGY MONEY AFUNGUKA FAMILIA ILIMFANYA APIGE PICHA ZA UTUPU

Msanii Gigy Money amesema sababu iliyomfanya apige picha za utupu ni kupata pesa ambazo anapeleka nyumbani kwao, licha ya kitendo hicho kutokuwa kizuri kwa jamii. 

Gigy Money amesema wazazi wake waliridhia kitendo hicho kwani pesa ambayo alikuwa anapata zinaenda nyumbani, na zilikuwa kwa ajili ya tangazo la...
nguo za ndani na sio vinginevyo.

“Mimi mama yangu, wazazi wangu na ndugu zangu fresh tu kwao kwa sababu nilikuwa napeleka hela nyumbani, sio kama nilikuwa nafanya vile bure, au nilikuwa namtangazia mtu makalio yangu hapana, nilikuwa nalipwa kutangaza brand ya nguo za ndani, ilikuwa ni rahisi kufanya kwa sababu nilikuwa napata hela”, alisema Gigy Money.

Gigy Money ambaye kwa sasa amepunguza mwili wake alipata umaarufu kwa kupiga picha za utupu ambazo zilileta gumzo kwa jamii, mpaka sasa ameamua kuingia kwenye muziki ili kujipatia kipato kwa shughuli ya halali.

0 comments:

Post a Comment