Pages

Subscribe:

Friday, October 13, 2017

JAY DEE: NI JAMBO JEMA WASANII KUPEANA USHIRIKIANO

Msanii Lady Jaydee ambaye hivi karibuni amepatana na aliyekuwa mhasimu wake msanii Mwana FA, amesema alishukuru sana kwa kitendo cha Mwana FA kumpa ushirikiano kwenye kazi zake na kupost Instagram kumpa promo. 

Akiongea Lady Jaydee amesema “Ni jambo jema msanii mwenzako anapokusuport, na ndio kitu ambacho wasanii wengi tunapenda, sisi binadamu kwa hivyo mkae ...
mkifahamu kwamba hakuna marefu yasiyo na ncha, nilishukuru kwamba msanii mwenzangu amenisuport”, amesema LadyJaydee.
 
LadyJaydee ameendelea kwa kusema kwamba.... “ni wasanii ambao tulikuwa tunaelewana, na ndio maana tuliweza kufanya nyimbo nyingi ambazo ziliweza kufanya vizuri, watu walikuwa wanasikitika kwa yale yaliyotokea”.

Wawili hao walikuwa kwenye bifu kali ambalo ilikuwa hata salamu hakuna, lakini hivi karibuni wameamua kuyamaliza na kuondoa tofauti zao.

0 comments:

Post a Comment