Pages

Subscribe:

Monday, October 2, 2017

MTANGAZAJI WA EFM DENNIS KUZIKWA SIKU YA KESHO

Mazishi ya aliyekuwa mtangazaji wa Efm radio ya jijini Dar es salaam, Dennis David Rupia, yanatarajiwa kufanyika Jumanne ya tarehe 3 Oktoba 2017, nyumbani kwao mkoani Morogoro.

Ratiba inaonyesha ibada ya kuaga mwili wa marehemu Dennis itafanyika katika kanisa katoliki Mwenge siku ya juma tatu tarehe 2 Oktoba, na kisha safari ya kuelekea Ifakara mkoani Morogoro itaanza kwa...
ajili ya mazishi.

Mkoani Morogoro kutakuwa na ibada ya kuaga mwili wa marehemu katika kanisa katoliki Kibaoni, na kisha kufuatiwa na ibada ya mazishi.

Dennis Rupia  amefariki tarehe 29 Septemba 2017 baada ya kuugua kwa muda mfupi.
 

0 comments:

Post a Comment