Pages

Subscribe:

Thursday, October 5, 2017

ROMELU LUKAKU AKANA MASHTAKA YA MAJIRANI ZAKE MAHAKAMANI

Great convo with @nba champ @money23green. God bless brother 💯 @manchesterunited @warriors  #MUFC #MUTOUR
Mshambuliaji wa Manchester United Romelu Lukaku amekana makosa ya kupiga kelele katika nyumba aliyokuwa akiishi baada ya kukamatwa nchini Marekani mapema mwaka huu.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 alishtakiwa kwa makosa hayo mnamo mwezi Julai baada ya maafisa wa polisi kupata malalamishi mengine matano ya kelele katika...
nyumba moja ya Beverly Hills.

Raia huyo wa Ubelgiji hakuwasili mahakamani mjini Los Angeles siku ya Jumatatu.
Wakili wake Robert Humphreys aliwasilisha ombi la kutokuwa na makosa hayo.
Kamishna Jane Godfrey aliahirisha kesi hiyo.

Baada ya kusikilizwa, wakili James Eckart alisema kuwa iwapo atapatikana na hatia, mshambuliaji huyo atakabiliwa na faini na kulipa fedha za gharama za simu zilizopigwa kwa siku tano, Lukaku anaweza kutowasili mahakamani yeye binafsi na badala yake anaweza kutumia wakili wake kumwakilisha.

Maafisa wa polisi wanasema walitoa tamko la onyo baada ya kupata wito kutoka kwa nyumba moja, Kisa hicho kilitokea wiki moja kabla ya Lukaku kujiunga na Manchester United kutoka Everton kwa kitita cha £75m.
 
Taarifa ya Beverly Hills wakati huohuo inasema kuwa Lukaku, ambaye alikuwa katika likizo Marekani ,aliwachiliwa katika eneo hilo kufuatia kisa hicho mnamo tarehe 2 mwezi Julai.

Amefunga mabao 11 katika mechi 10 za United.

0 comments:

Post a Comment