Pages

Subscribe:

Thursday, October 5, 2017

SHOW ZAWA CHANZO CHA ASLAY KUACHIA NYIMBO MFURULIZO

#nguvuyaumma #tigofiesta2017
Msanii wa muziki wa bongo fleva Aslay, ambaye sasa hivi anakimbiza kwenye game kwa kuachia kazi mpya mara kwa mara na zenye ubora, amesema sababu ya yeye kufanya hivyo ni kupata kazi nyingi zitakazombeba kwenye show. 


Akizungumza Aslay amesema siku za nyuma alikuwa anategemea kundi kumbeba, lakini kwa sasa yupo mwenyewe lazima awe na kazi nyingi ambazo zitamfanya apate show na...
kufanya vizuri jukwani.

“Tangu nimetoka kwenye kundi nimekuwa nafanya kazi mimi kama mimi, kwa hiyo nategemea show zangu mimi ziwe na nyimbo zangu tu sio za bendi, ndio mana natoa nyimbo nyingi ili mradi nipate show na kutumia nyimbo zangu na sio za bendi”.

Aslay pia amesema sababu nyingine ya yeye kuachia kazi mpya mara kwa mara ni kwa sababu ya wingi wa kazi nzuri alizonazo, hivyo anahofia iwapo haitatoka mtu mwengine atatoa nyimbo nzuri zaidi yake na kuipoteza.

0 comments:

Post a Comment